29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ramos: Ningejua ningepewa kadi mapema

Sergio RamosBARCELONA, HISPANIA

BAADA ya Real Madrid kufanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Barcelona juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania, beki wa timu hiyo, Sergio Ramos, amedai kwamba angejua kama klabu yake itashinda huku ikiwa na watu 10 uwanjani basi angepewa kadi nyekundu mapema.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Comp Nou, Barcelona walipewa nafasi kubwa ya kushinda hasa kutokana na ubora wao kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Lionel Messi, Suarez na Neymar.

Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti kwa Barcelona na kujikuta wakipokea kichapo huku wapinzani wakiwa pungufu baada ya Ramos kuonyeshwa kadi nyekundu na kuwaacha wenzake wakiwa 10 lakini walifanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Kama ningejua kwamba tunaweza kushinda mchezo huo, basi ningeweza kupata kadi nyekundu mapema sana na kuwaacha wachezaji 10 wakipata ushindi huo.

“Ninaamini kwamba kikosi chetu kilikuwa bora bila ya kujali ya kuwa pungufu, lakini tuliweza kufanya vizuri ugenini,” alisema Ramos.

Katika mchezo huo wenyeji Barcelona walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza ambalo liliwekwa wavuni na beki wao, Gerard Pique, katika dakika ya 56 kwa kichwa baada ya kupigwa kona, lakini mshambuliaji wa Madrid, Karim Benzema, alisawazisha bao hilo kabla ya Cristiano Ronaldo kuongeza la pili.

Hata hivyo, Barcelona bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 76 ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye pointi 70 huku Real Madrid ikiwa na pointi 69.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles