Nyota AC Milan afariki dunia

0
708

stream_imgMILAN, ITALIA

NYOTA wa zamani wa klabu ya AC Milan na kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Casare Maldini, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa anaitumikia klabu hiyo ya Italia na kuchukua mataji manne ya Ligi Kuu, Kombe la European, Coppa Italia, baada ya kustaafu soka aliamua kuwa kocha na kuifundisha timu ya Taifa Italia.

Familia ya mchezaji huyo imethibitisha kifo chake ambacho kilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini Trieste nchini Italia, lakini familia hiyo hadi sasa haijaweka wazi chanzo cha kifo hicho.

Klabu ya AC Milan imesikitishwa na kifo cha nyota huyo na kudai itaungana na familia katika kipindi hiki kigumu hasa kutokana na mchango wake katika soka la nchini Italia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here