26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wema Sepetu: Habari za Wema Sepetu kuanza kupatikana kesho

wema-sepetu-1NA FESTO POLEA

MFUMO wa huduma ya simu utakaokuwa na habari zote za staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu, utaanza kupatikana Ijumaa ya kesho kwa kuwawezesha mashabiki wake kuipakua ‘application’ hiyo.

Wema aliweka wazi hayo juzi alipotembelea Ofisi za New Habari (2006) Ltd zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African.

“Application hiyo itakuwa tayari (kudownlod) kupakuliwa kuanzia Ijumaa (kesho) na wanaotaka kupata habari za Wema Sepetu wanatakiwa kuandika Wema kisha wanatuma kwenda 15404 hii ni kwa mitandao yote ya simu, humo kuna kila kitu kinachohusu maisha yangu.’’

Naye meneja wa mrembo huyo, Martin Kadinda, alifafanua zaidi kwamba mfumo huo upo katika sehemu tatu ikiwemo ya ujumbe mfupi (sms) kwa simu yoyote, (kudownlod) kupakua pamoja na kutumia vifaa vyenye uwezo wa intaneti ikiwemo kompyuta, Ipad na vifaa vingine kama hivyo.

“Kwa sasa ‘application’ hiyo inapitia katika simu tv ndiyo kuna ‘application’ ya Wema Sepetu. Wema amekuwa na vitu vingi na marafiki wengi lakini alikuwa hajui namna ya kujitengenezea fedha hivyo tukaona tuje na mfumo huu wa kiteknolojia ili aweze kujiongezea kipato,’’ alieleza Kadinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles