26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wolper ateswa na picha zake za utupu

Jackline-Wolper-2*Amwita Diamond baba mkwe

GEORGE KAYALA NA THERESIA GASPER

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amejikuta akimwaga machozi alipokuwa akisimulia mkasa kati yake na aliyekuwa mchumba wake raia wa Kongo, DR.

Akizungumza kwa hisia kali katika kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema, alisema kabla ya kuachana na mwanaume huyo wa Kongo alipigwa picha za utupu kwa madai kuwa atakuwa akiziangalia kipindi atakachokuwa peke yake jambo ambalo hakuliafiki.

Wolper alieleza zaidi kwamba licha ya picha hizo kupigwa kitu kingine kilichoumiza moyo wake ni pale alipobaini kwamba huyo Mkongo alikuwa mume wa mtu, hivyo aliamua kuachana naye licha ya vitisho vya kuchafuliwa na picha hizo alizopigwa.

“Kabla ya kuachana naye alikuwa na tabia ya kunipiga picha za utupu, baadhi nilizifuta lakini baada ya kuachana akasema kwamba kuna kitu atakifanya ambacho sitaamini, nahisi zitakuwa ni hizo picha,” alieleza Wolper.

Hata hivyo, alisema amewasiliana na mwanasheria wake juu ya jambo hilo ili ikitokea mwanaume huyo akaamua kumchafua kwa kusambaza picha hizo za utupu sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Wolper amefunguka kuwa kwa sasa Abdul Nasib ‘Diamond’ ni kama baba mkwe wake baada ya kuwa na mahusiano na msanii aliye chini ya lebo yake ya Wasafi, ‘Harmonize’.

Wolper alisema mambo ya zamani yameshapita na sasa wanaangalia maisha ya mbele.

 

 

“Sasa hivi namheshimu Diamond kama baba mkwe wangu ukizingatia ni mtu anayesimamia kazi za Harmonize na alishatupa baraka zote katika mapenzi yetu.

 

“Sijali maneno ya watu wanaoongelea uhusiano wangu kwamba nipo na msanii mdogo mwenye nyimbo mbili tu, sijali mimi nachojali ni mapenzi ya kweli,’’ alieleza.

 

 

Naye Harmonize aliweka wazi kwamba kwa sasa ametulia kimapenzi na Wolper na hakuwahi kumkuta na pete wala mpenzi hivyo haoni shida kuwa na Wolper licha ya kuwa na umri mkubwa kuliko wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles