MKALI wa muziki wa hip hop wa kundi la Young Money, Lil Wayne, ameitukana kampuni ya Cash Money Records kwa madai kwamba hadi sasa hajalipwa fedha zake kutoka kwa bosi wa kundi hilo, Birdman.
Msanii huyo alikuwa akiidai kampuni hiyo kiasi cha dola milioni 51 walizokubaliana kwa ajili ya kuwasimamia wasanii wanaofanya kazi nao.
Awali msanii huyo alijitoa katika kundi hilo kutokana na deni hilo, ila walikuja kumalizana na Birdman kwa makubaliano na ndipo msanii huyo akarudi kundini lakini amelalamika kutokulipwa.