30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Mambo ya Nje Iran ajiuzulu

TEHRAN, IRAN

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, aliyeongoza mazungumzo ya kufikiwa kwa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa mengine matano yenye nguvu duniani, amejiuzulu ghafla.

Zarif ametangaza kujiuzulu na kuliomba radhi taifa kwa kuchukua hatua hiyo ghafla.

Zarif aliandika taarifa ya kujiuzulu kupitia ukurasa wake wa twitter juzi usiku.

Shirika la Habari la DPA limearifu kwamba pamoja na Rais Hassan Rouhani mapema jana kuthibitisha kujiuzulu kwa Zarif, hatakubaliana na ombi hilo.

Miito imeongezeka kwa Rais Rouhani kutoka kwa wabunge wa Iran na wenye ushawishi mkubwa ya kulikataa ombi hilo la Zarif.

Taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa ofisi ya rais imesema kuwa Zarif hatakuwa peke yake, Serikali itamuunga mkono

Zarif ameitumikia wizara hiyo tangu Agosti 2013, na katika kipindi hicho amekuwa akikabiliwa na shinikizo la mara kwa mara kutoka kwa wanasiasa wenye mrengo mkali wanaoipinga sera yake ya kuelegeza misimamo ya kiuhusiano na mataifa ya Magharibi.

Sababu ya kujiuzulu kwake imeibua mjadala mzito kwenye majukwaa ya kijamii, huku baadhi wakidai amechoshwa na ukosoaji kutoka kwa wenye misimamo mikali, kuhusu mkataba huo wa nyuklia pamoja na sera yake hiyo kuelekea mataifa ya magharibi.

Aidha wengine wanadai ameghadhibishwa na namna alivyowekwa pembeni katika mkutano na Rais wa Syria, Bashar al-Assad juzi.

Kwa ujumla wanakubaliana kwamba kujiuzulu kwake huenda kukamaanisha kumalizika kwa haraka kwa makubalino hayo ya nyuklia yaliyowezesha Iran kuondolewa vikwazo, ambayo hata hivyo tayari yalikumbwa na pigo baada ya Marekani kujiondoa mwaka jana.

Wachambuzi waliopo Tehran wanaamini Iran haitaweza kuziba pengo la Zarif na mtu mwenye misimamo, haiba na uzoefu kama wake, si naibu wake Abbas Araghchi au Ali-Akbar Salehi, ambaye ni mkuu wa shirika la nyuklia la Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles