31.9 C
Dar es Salaam
Sunday, January 16, 2022

Kiongozi Vatican akutwa na hatia ya unyanyasaji watoto kingono

VATICAN CITY, VATICAN

WAZIRI wa Uchumi wa Vatican na mshauri wa Papa Francis, Kardinali George Pell (59) amekutwa na hatia ya kuwadhalilisha kingono wavulana wawili waliokuwa wakiimba kwaya.

Mahakama ya Australia jana ilisema Kardinali Pell amekutwa na hatia ya makosa matano ya udhalilishaji.

Moja ni la kuwadhalilisha kingono watoto na manne ya kuwadhalilisha kinyume cha maadili wavulana waliokuwa na umri wa miaka 13 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick mjini Melbourne katika miaka ya 1990.

Jopo la majaji 12 kwa pamoja lilimkuta na hatia Desemba 11 mwaka jana, lakini jaji kiongozi aliamuru kuzuia kuripoti kesi hiyo tangu ilipoanza Mei mwaka jana.

Amri hiyo imeondolewa jana baada ya waendesha mashtaka kuamua kutoendelea na kesi nyingine ya pili ya madai kama hayo ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya kardinali huyo.

Adhabu ya makosa kama hayo ni kifungo cha hadi miaka 50 gerezani. Kikao cha kusikiliza hukumu kinaanza leo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,603FollowersFollow
530,000SubscribersSubscribe

Latest Articles