23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI WA KAZI ZANZIBAR AKACHA KIKAO NA WADAU SEKTA BINAFSI

KIKAO cha Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Maudline Castico na wadau wa sekta binafsi kimesambaratika baada ya waziri huyo kudaiwa kukacha kikao hicho.

Kikao hicho alichokiitisha waziri huyo Julai 24, mwaka huu, kilikuwa na ajenda ya kujadili nyongeza ya mishahara ya kima cha chini ya wafanyakazi visiwani Zanzibar ambayo Julai mwaka huu ilipandishwa kuwa Sh 500,000 sawa na asilimia 109 ambayo imeonekana kuwa gumu kwa sekta binafsi.

Akizungumza baada ya kutangaziwa waziri hatakuwapo katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara visiwani humo, Taufiq Turuki, alisema wameshangazwa na hatua ya waziri huyo kukacha katika kikao alichokiitisha mwenyewe na wadau hao.

Alisema katika kikao hicho walijipanga kumweleza waziri huyo athari za kuendelea na kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi visiwani humo ambayo haiendani na hali halisi ya uchumi visiwani humo kulinganisha na Tanzania Bara.

“Tumeshangazwa na kusikitishwa na hatua ya waziri kukacha kikao hiki ambacho bila yeye tusingekuwapo hapa, cha ajabu zaidi anakuja Katibu Mkuu wake anatuletea kanuni ambazo hata hazihusiani na kikao chenyewe.

“Tulikubaliana kwamba kima cha chini hakiendani na hali halisi ya uchumi ambao ni mdogo visiwani Zanzibar, akasema atatuita ili tuzungumze naye kisha anatukimbia, hatumuelewi,” alisema Turuki.

Aidha, alisema kwa hatua hiyo Zanzibar itarudi katika sekta isiyo rasmi ambapo mwenye uwezo atalipa mishahara hiyo na asiye na uwezo ataajiri vibarua lakini pia madhumuni ya kupigania jambo hilo ambalo limechukua zaidi ya miaka 50 wakaweza lakini wamerudishwa nyuma hatua nyingi.

Hivi karibuni, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, ilitangaza kima kipya cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi Zanzibar, kuanzia Julai Mosi mwaka huu chini ya kifungu cha 97 (1) cha sheria ya ajira Na. 11, ya mwaka 2005.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles