28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Ummy asisitiza elimu kwa wakulima

 MWANDISHI WETU– MOROGORO

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aimeipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuwasaidia wakulima kwa changamotombalimbali wanazokabiliana nazo.

Waziri Ummy ametoa pongezi hiyo jana alipotembelea Banda la Benki ya NMB katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoa wa Morogoro. Awali akimkaribisha Waziri Ummy kwenye Banda la NMB, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki, Harold Lambileki, ambapo alisema benki hiyo ipo bega kwa bega na Serikali katika kusaidia sekta ya kilimo kwa ujumla.

Alisema tangu mwaka 2016 hadi sasa NMB imetoa kwa wakulima zaidi ya Sh bilioni 800 nchi nzima ili kuwasaidia wakulima kwenye mnyororo mzima wa kuongeza thamani dhidi ya mazao yao katika maeneo mbalimbali.

Alibainisha kuwa kiwango hicho cha fedha kimejikita kuanzia mkulima anapoandaa mashamba, pembejeo, uvunaji na uhifadhi na baadaye usafirishaji wa mazao ili kupunguza baadhi ya changamoto za awali kwenye sekta hiyo.

Aidha alimweleza Waziri Ummy kwa mwaka huu pia NMB imetenga zaidi ya Sh bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao nchi nzima kwa vyama vya wakulima, AMCOS na pia kwa mkulima mmoja mmoja wote watafaidika kwa utaratibu ambao umewekwa na benki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles