24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi tatu zashawishi uchaguzi Marekani usogezwe mbele

 WASHINGTON, MAREKANI

NCHI za China, Urusi na Iran, ni kati ya nchi zinazotaka kushawishi uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu, mkuu wa idara ya intelijensia nchini Marekani ametahadharisha.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara hiyo ilisema nchi za kigeni zilikuwa zinatumia ‘’njia za ushawish’’ kuyumbisha kura.

Ilisema China haikutaka kuchaguliwa tena kwa Rais Donald Trump, huku Urusi nayo ilitaka kumuumiza Joe Biden wa Chama cha Democrat.

Wakuu wa ujasusi wanaishutumu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Wanasema Urusi ilitaka kusaidia kuongezea nguvu kampeni ya Rais Trump,ikiwamo kueneza habari za uongo mtandaoni. Urusi imekana madai hayo.

Alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa alichopanga kufanya kuhusu ripoti kuhusu kuingilia uchaguzi, Rais Trump alisema utawala wake utaangalia “kwa karibu” suala hilo.

Tangazo hilo linakuja wakati kukiwa na madai ya Trump kuhusu hatari ya kupigiwa kura ya posta au barua pepe.

Alidai uchaguzi uahirishwe ili kuzuia ‘’uchaguzi wa udanganyifu kuwahi kutokea katika historia,’’ kauli iliyosababisha upinzani hata miongoni mwa wanachama wa chama chake.

Rais Trump wa Chama cha Republican, anasaka ushindi wa awamu ya pili ya miaka minne madarakani.

Mkuu wa Kituo cha kitaifa cha Usalama na Kupambana na Ujasusi (NCSC), William Evanina, alitoa taarifa hiyo Ijumaa.

Nchi za kigeni zinajaribu kupendelea matakwa ya wapiga kura, kubadilisha sera za Marekani, “kuongeza mizozo” nchini “na kudhoofisha imani ya watu wa Marekani katika mchakato wetu wa demokrasia”, Evanina.

Alisema itakuwa vigumu hata hivyo kwa maaduo kuingilia kati na kudhibiti upigaji kura na matokeo,

Nchi nyingi ‘’zina upendeleo kuhusu nani ashinde uchaguzi’’, alisema, mkurugenzi wa kupambana na ujasusi amesemema ‘’ awali wanazitazama’’ China, Urusi na Iran: 

China ‘’inapenda kuona Trump akikikosa kiti hicho ‘’ taarifa hiyo imeeleza na kuongeza kuwa China imekuwa ‘’ikiongeza jitihada za ushawishi’’ kabla ya kura. 

Urusi inatafuta kupaka matope nafasi anayoiwania Biden, huku washirika wenye uhusiano na Urusi ‘’ pia wanatafuta kumpiga jeki Trump kwenye mitandao ya kijamii na televisheni’’Iran inajaribu ‘’ kudhoofisha taasisi za chama cha Democratic Marekani ‘’, bwana Trump na ‘’kuigawanya nchi’’ kwa kusambaza taarifa za uongo na ‘’maudhui kuipinga Marekani ‘’ mtandaoni. Jitihada zao zinasukumwa na imani kuwa muhula wa pili wa rais ‘’ utasababisha muendelezo wa shinikizo la Marekani juu ya jitihada za kuchochea mabadiliko ya utawala,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles