23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri: Sheria umiliki silaha iangaliwe upya

magheNA ESTHER MNYIKA ,DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maliasili na Utalii , Profesa Jumanne Maghembe ameishauri Serikali  kuangalia upya endapo bado  kuna sababu za msingi kwa wananchi kuendelea  kununua na kumiliki bunduki  zenye mitutu mikubwa.

Ametoa ushauri huo kutokana  na kuongezeka     matukio ya  kukamatwa  kwa silaha  zikiwa zinatumika katika  vitendo vya uhalifu nje ya mikono ya wamiliki halali wa silaha hizo.

Mbali na Profesa Maghembe, Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP), Ernest Mangu, alisema umefanyika uchunguzi na kubaini wanaomiliki silaha wanazikodisha kwa majangili.

Alisema jeshi la polisi linatarajia kuendesha operesheni  maalum nchi nzima kwa lengo la kudhibiti  matumizi mabaya ya silaha kwa wananchi wanaozimiliki.

“Miaka iliyopita wananchi walikuwa waaminifu…  kwa sasa baadhi baadhi yao  wanaihujumu Serikali kwa kufanya biashara ya kukodisha silaha kwa majangili,”alisema IGP Mangu.

Profesa Maghembe alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Waziri  pia  aliupongeza  uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu uliosaidia kukamata majangili wanaodaiwa kuhusika na tukio la kutunguliwa helikopta ya doria Januari 29 mwaka huu.

Majangili hao wanadaiwa kushambulia helikopta iliyokuwa inafanya doria  katika   pori  la akiba  Maswa na ranchi ya Wanyamapori ya Mwiba.

Tukio hilo  lilisababisha   kifo cha rubani  Rogers Gower raia wa Uingereza huku  Nick Desta aliyekuwa pamoja na Rogers akinusurika na kukumbizwa  Nairobi kwa matibabu .

Profesa Magembe alisema tukio hilo limetoa funzo kubwa  kwa nchi na linadhihirisha kwamba baadhi ya  majangili wamefika hatua ya kujijengea uthubutu na ujasiri wa kutisha.

“Kutokana  na mazingira hayo  wizara yangu  imeamua kurejea kwa haraka na kwa upana  zaidi mbinu na mikakati  yake dhidi ya ujangili wa wanyamapori na mazao ya misitu    na usafirishaji  haramu  wa mazao ya wanyamapori,” alisema.

Aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuimarisha na kuunda haraka  kikosi maalum  cha kupambana na uhalifu  wa  wanyamapori.

“Kikosi hiki kitaundwa  kwa kushirikiana  na taasisi zote  za wizara  kama Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya Usimamizi  wa Wnyamapori  Tanzania (TAWA), Hifadhi  za Taifa (TANAPA) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),” alisema Waziri Maghembe.

Alisema kuanzia sasa  majangili watatafutwa  kwa kutumia teknolojia akisisitiza kuwa hakuna operesheni tokomeza  tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles