24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kodi si kuwakomoa wafanyabiashara’

Philip-MpangoNA FLORIAN MASINDE,DAR ES SALAAM.

SERIKALI imesema hatua yake ya kukusanya kodi isitafsiriwe kuwa ni kuwakomoa wafanyabiashara bali ni katika kuhakikisha nchi inajikwamua kuelekea kwenye uchumi wa kati.

Ufafanuzi huo ulitolewa   Dar es Salaam jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Balozi Philip Mpango alipozungumza na wafanyabiashara.

Alisema mpango wa Serikali ni kuiwezesha nchi  kujiendesha katika uchumi na siyo kuwanyanyasa wafanyabiashara kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu.

Kipaumbele cha kwanza cha serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi ili fedha na rasilimali za umma ziweze kutumika ilivyokusudiwa na kuifikisha nchi kwenye kipato cha kati.

Mpango alisema mwelekeo wa Serikali katika uchumi katika mwaka ujao wa fedha ni huduma bora zinazotegemea mapato yanayotokana na kodi.

“Serikali inatambua umuhimu  wenu katika kuinua uchumi wa nchi hivyo kupitia Wizara ya Fedha tutafanya kazi kwa karibu zaidi  kuwezasha taifa kuacha kuwategemea wahisani katika kujiendesha kwa uchumi.

“Serikali imejipanga kuwajengea mazingira ya kufanya shughuli zenu bila kubughudhiwa kwani nyie ndiyo mnaosaidia taifa kutoa ajira na kulipa kodi stahiki,” alisema Balozi Mpango.

Mpango sema mpango wa maendeleo ya miaka mitano utakamilika ifikapo mwishoni mwa Juni na nchi kuwa katika mikakati ya kujenga uchumi wa viwanda kwa ujenzi na kufufua viwanda vinavyotumia mali ghafi zilizopo nchini na viwanda vunavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na wananchi kwa mahitaji muhimu.

Alisema Serikali imepanga kuanzisha miradi mikubwa itakayokamilika kwa wakati na muda mfupi  na ujenzi wa reli ya kati hivyo wafanyabiashara kuwa sehemu ya watakaofanikisha mpango huo.

Waziri alisema  wafanyabiashara wanatakiwa kufanya usajili wa walipa kodi na kupata namba ya mlipa kodi,   kuwa na tabia ya kutunza kumbukumbu za mauzo na gharama za uendeshaji,  kuendelea kutumia mashine za kulipia za eletroniki na kutoa risiti kwa wanunuzi.

Nao wafanyabiashara wameitaka Serikali kuingalia kwa ukaribu zaidi sekta ya kilimo  ikizingatiwa hakuna taifa linaloweza kuendelea katika uchumi duniani bila kutegemea kilimo.

Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Taifa, Yusufu Sinare, alisema asilimia 75 ya Watanzania wanategemea sekta hiyo katika kuendesha maisha yao hivyo viwanda na wafanyabiashara wanategemea zaidi bidhaa zinazotokana na kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles