24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI NAPE AKEMEA UDANGANYIFU MICHEZONI

NA OSCAR ASSENGA, TANGA


nape-nnauye-2WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amekemea vikali baadhi ya tabia za viongozi wa timu zinazoshiriki michezo mbalimbali nchini kutumia wachezaji wasiostahili kutumika katika mashindanohusika.

Waziri huyo  aliyasema hayo wakati akizindua mashindano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma na Binafsi (Shimmuta), yanayoendelea Jijini Tanga, ambayo yameshirikisha timu mbalimbali kutoka mashirika ya umma na binafsi Tanzania.

Nnauye aliwataka pia viongozi wa shirikisho hilo kufanya uhakiki upya wa wachezaji wa timu shiriki ili kuondoa lawama zinazoweza kutokea na kupata mshindi anayestahili kwa kufuata sheria na taratibu zote za mashindano.

“Nawaomba viongozi muangalie na kupitia upya wachezaji wa timu shirikiili kusiwe na zengwe lolote katika mashindano haya na mshindi katikakila mchezo apatikane kihalali,” alisisitiza Nnauye.

Aidha, ametoa wito kwa mashirika kutenga muda na fedha ili kuwezesha timu zao kushiriki katika michezo, ikiwa ni moja ya kujenga mshikamano na amani kwa Watanzania na pia kujenga afya ya mwili na akili.

Awali akisoma taarifa ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Shimmuta, Hamisi Mkanachi, alisema mashindano hayo msimu huu yameshirikisha zaidi ya timu 10 na kumuomba Waziri Nape awasaidie kuliongoza shirikisho hilo kwa kusaidia taasisi kushiriki michezo kwenye maeneo yao ya kazi.

Nape alisema suala la mamluki kuwepo kwenye mashindano hayo watajitahidi kukabiliana nalo kwa kuhakikisha linakwisha kabisa, kwani nia ya michezo hiyo ni kuonyesha vipaji vyao, wakitumia pia kama sehemu ya kufahamiana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles