23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TUJIANDAE KUISHUHUDIA MAREKANI YA GOFU

Na MARTIN MAZUGWA


barack-obama-donald-trumpKILA mwanadamu ana mapenzi ya mchezo anaoutaka, lakini mchezo unaopendwa zaidi duniani ni soka.

Soka imekuwa na mashabiki wengi, licha ya kuwepo michezo mingine kama pete, riadha, kikapu, gofu na mingineyo.

Marekani ni taifa kubwa na ukubwa wake hautokani na mita za mraba pekee, bali hata katika mambo ya kiuchumi ipo juu sambamba na China, Japan, Urusi na India, ambayo ni mataifa bora zaidi duniani.

Licha ya kujikita katika kukuza na kuimarisha uchumi wa n hi zao, lakini bado wamekuwa na mchango mkubwa katika michezo.

Kutokana na kutambua umuhimu wa michezo, Marekani imeanza kuwekeza katika michezo mbalimbali ili kuzidi kujiimarisha katika nyanja zote,  ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, gofu pamoja na kikapu, ambao ndio unaongoza kwa kupendwa nchini humo.

Kutokana na kutaka mabadiliko katika michezo, tayari wamemuondoa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Jurgen Klinsman, kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Nchi hiyo ilifanya uchaguzi na kumpata rais wa 45 katika historia ya taifa, ambapo Donald Trump amepata nafasi ya kuliongoza taifa hilo kubwa duniani.

Mapenzi ni kitu tofauti, kila mwanadamu ameumbiwa, japokuwa hayafanani, licha ya kuwa na lengo moja la kuleta maendeleo katika taifa. Trump na mtangulizi wake, Barack Obama, wanatofautiana katika vitu wanavyopenda, hususan michezo.

Mafahali hawa wawili, licha ya kutofautiana katika mitizamo yao ya kiuongozi, hata kwa upande wa michezo wanayovutiwa nayo wamekuwa tofauti.

Bilionea Trump amekuwa akiwekeza na kuutumia muda wake wa mapumziko katika mchezo wa gofu, ambao umekuwa ukijizolea sifa kubwa ulimwenguni kote.

Trump amekuwa akivutiwa na wacheza gofu  kama Tiger Woods, Phil Michelson, Rory Mcllroy, Adam Scot na Jordan Spieth, ambao ni kati ya nyota wanaopendwa na wapenzi wa mchezo wa gofu duniani kutokana na ubora wao.

Licha ya kuupenda mchezo wa gofu, Trump pia ni shabiki wa mchezo wa tenisi, ambapo anamiliki uwanja wa ndani wa mchezo huo ambao umejengwa kwa gharama kubwa.

Mbali na tenisi, Trump anamiliki kituo cha mchezo wa gofu kinachoitwa Trump National Golf Club, kilichopo Washington, D.C ambacho mwakani kitatumika katika michuano mikubwa ya mchezo huo.

Kutokana na kutingwa na shughuli mbalimbali, mara ya mwisho Trump alionekana katika mchezo wa gofu  miaka kumi iliyopita huko Mar-a-Lago, katika ufukwe wa Miami, alipocheza dhidi ya Johan Kriek, bingwa wa taji la  Gland Slams, ambapo walicheza mchezo wa hisani wa kuchangia wagonjwa wa kansa ambapo kiasi cha Euro milioni 1.6 zilikusanywa katika mchezo huo.

Kwa upande wa Obama, amekuwa akivutiwa na nyota kama vile Stephen Curry, Dwayne Wade, Kobe Bryant, Michael Jordan, Lebron James  na wengine wengi wanaotamba katika mpira wa kikapu ambao umekuwa ukipanda siku hadi siku.

Obama ameshindwa kuficha hisia zake juu ya mchezo wa kikapu mara baada ya kuialika Ikulu timu ya Cleverland Cavaliers, ambao ndio mabingwa wa NBA msimu uliopita kwenda kula chakula cha pamoja.

Rais huyo, mara nyingi alikuwa akionekana katika viwanja tofauti vya mchezo wa kikapu akishuhudia mchezo huo unaopendwa zaidi nchini humo.

Obama, ambaye ni shabiki mkubwa wa Chicago Bulls, aliwahi kukaririwa akisema analazimika kuishabikia Washington Wizards kutokana na yeye kuishi katika jimbo hilo.

Mbali na hiyo, katika moja ya mazungumzo aliyowahi kufanya rais huyo, alikiri kuwa siku moja anataka kuwa mmiliki wa timu moja inayoshiriki Ligi Kuu ya NBA na kuwaacha wadau wakiwa na maswali kuwa ni timu ipi anayotaka kuinunua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles