24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu azindua vibali vya kielektroniki

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka watakaopewa vibali vya ukaazi vya kielektroniki kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 26, wakati akizindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

“Utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususani katika sekta ya viwanda kwani hatua itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

“Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo na wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo,” amesema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles