28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa.

Na MWANDISHI WETU,

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amezindua mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Jobaj, Wilaya ya Karatu mkoani Manyara, unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania.

Mradi huo wenye thamani ya Sh milioni 285, ulizinduliwa juzi wakati wa ziara ya kiongozi huyo mkoani hapa na utahudumia vijiji vitatu vya Kata ya Baray ambavyo ni Mbunga Nyekundu, Jobaj na Dumbechand.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wananchi wautunze ili uweze kudumu kwa muda mrefu.

“Nawaomba muutunze mradi huu kwa sababu kama utadumu kwa muda mrefu, ile kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili itakuwa imeondolewa,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania, Revocutus Kamara, alisema mradi huo unatokana na mahitaji ya maji katika vijiji hivyo vitatu na uwepo wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2009.

“Mradi huu wa maji unatekelezwa kwa awamu tatu. Awamu ya kwanza ilianza Machi hadi Novemba 2016, ambapo  wakazi 5,272 ikiwa ni pamoja na taasisi nne za Serikali ambazo ni zahanati, magereza, shule ya msingi na sekondari zilizoko katika Kijiji cha Jobaj, wananufaika kwa kupata maji safi na salama.

“Awamu ya pili na ya tatu ya mradi huo itaanza Desemba hii, na itagharimu zaidi ya Sh milioni 200,” alisema Kamara.

Akizungumza kuhusu mradi wa umwagiliaji, mkurugenzi huyo alisema shirika lao limechangia kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga kilomita 1.716 za mfereji katika Kijiji cha Jobaj.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles