24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

BAYPORT KUBORESHA UTENDAJI KAZI SERIKALINI

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akikabidhi moja ya kompyuta kwa Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora, Angelah Kairuki. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akikabidhi moja ya kompyuta kwa Waziri
wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora, Angelah Kairuki. Kushoto ni Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo.

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KUKUA kwa sayansi na teknolojia kumerahisisha utoaji huduma mbalimbali hususan katika ofisi za umma.

Leo hii si Tanzania tu ila dunia yote inahitaji matumizi makubwa ya kompyuta katika kusaidia utendaji kazi wa uhakika wenye tija katika eneo husika.

Kutokana na umuhimu huo wa kompyuta duniani kunafanya bidhaa hizo kupatikana kwa bei ghali, ukiacha zile za gharama nafuu ambazo kwa kiasi fulani huwa hazina ubora na zinaweza kuathiri badala ya kujenga kama ilivyokusudiwa.

Umuhimu huo unaifanya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kununua kompyuta 205 za aina mbalimbali na kuikabidhi serikali.

Makabidhiano ya kompyuta hizo zenye thamani ya Sh milioni 500 yalifanyika mwanzoni mwa wiki ambapo Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, ndiye aliyezipokea.

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, anasema kompyuta hizo zitarahisisha utoaji huduma serikalini ambapo kompyuta 125 zitabaki Makao Makuu ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kompyuta 80 zitagawanywa na wizara yenyewe kwa kuangalia mahitaji ya ofisi zao.

Anasema kutoa kompyuta hizo ni mkakati wao wa kusaidia jamii katika sekta mbalimbali, ikiwa ni matokeo mazuri ya kuungwa mkono na Watanzania tangu taasisi hiyo ilipoanza kutoa huduma zake mwaka 2006.

“Tunafanya kazi zetu kwa ufanisi, tunatoa mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na wengi wameendelea kutuunga mkono hali inayoifanya taasisi yetu ipige hatua kubwa kwenye sekta za mikopo.

“Hii inatufanya tupate mawazo ya kushirikiana na serikali yetu kwa undani zaidi kwa kusaidia kazi mbalimbali za kijamii, pamoja na misaada ya kuboresha utendaji kazi serikalini kama tulivyofanya kwa kutoa kompyuta hizi,” anasema Mbaga.

Anasema lengo lao ni kutoa huduma bora ya kuwezesha wateja na wananchi wote kiuchumi kwa kuwakopesha fedha ili wazitumie kuanzisha na kuendeleza biashara zao kwa ajili ya kuongeza chanzo kipya cha mapato na kuacha kutegemea mshahara kwa wale walioajiriwa serikalini.

Ukiacha ukopeshaji wa fedha unaondeshwa kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa, pia alielezea umuhimu wa huduma wanazotoa, hususan mikopo ya viwanja vinavyohusu Watanzania wote.

Anasema yoyote anaweza kukopeshwa viwanja vyenye hati ambapo lengo ni kusaidia jamii kupata ardhi inayopanda thamani siku hadi siku kwa utaratibu nafuu.

“Bado taasisi yetu ina huduma nyingi zenye lengo la kusaidia wateja wao kujikwamua kiuchumi, hivyo Watanzania waendelee kutuunga mkono.

“Tunazo huduma za mikopo ya fedha kwa njia ya simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’, bima ya elimu kwa uwapendao ambapo huduma zote hizo zinapatikana kwa utaratibu rahisi kwa kupitia matawi yetu 82 yaliyoenea katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, pamoja na mawakala wetu zaidi ya 1000,” Anasema.

Anasema wateja wao pia wanaweza kutembelea mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz ambao unaonyesha namna wanavyotoa huduma zao kwa kiwango bora.

Naye Waziri Kairuki anasema, msaada huo utapunguza changamoto za ukosefu wa kompyuta katika baadhi ya ofisi za serikali nchini.

“Hiki ni kitendo cha kiungwana na kinachostahili kuigwa na taasisi zote nchini kwa sababu kutoa kompyuta 205 ni msaada mkubwa mno kwetu.

“Kompyuta hizi zitasambazwa katika maeneo yenye changamoto husika ili kuhakikisha watumishi wetu wanafanya kazi kwa moyo na kuleta maendeleo,” anasema Kairuki.

Waziri Kairuki anasema kutokana na mahitaji ya serikali na uanzishwaji wa maeneo mengine ya kiserikali kuna uhitaji mkubwa wa vitendea kazi hivyo.

Anasema maeneo ya wilaya mpya na halmashauri nazo zina uhitaji huo, hivyo wataangalia namna bora ya kusambaza kompyuta hizo ili ziwe na tija na kurahisisha utoaji wa huduma kwa watumishi wa umma.

Waziri Kairuki anawashukuru Bayport huku akiwaasa waendelee kutoa huduma bora pamoja na kubuni huduma ambazo zinaweza kuwa na tija kwa nchi.

“Tunawaomba Bayport msiishie hapa tu, endeleeni kushirikiana na serikali kwa kutusaidia katika mambo mbalimbali kwani serikali haiwezi kufanya kila jambo kwa wakati, hivyo wadau kama nyie mna umuhimu mkubwa,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles