23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAISLAMU KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum

Na PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM

WAISLAMU wanatarajia kufanya maandamano ya amani ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) yatakayofanyika Desemba 10.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Sheikh wa Mkoa, Alhad Mussa, alisema maandamano hayo yataanzia viwanja vya Mnazi Mmoja, kuelekea barabara ya Morogoro, Msimbazi, Uhuru na Lumumba na kurudi kwenye viwanja hivyo.

Alisema viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya siasa na Serikali pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini  wataungana na Waislamu kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume.

Alisema mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

“Desemba 11, mwaka huu kutakuwa na sherehe za maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad, hivyo basi Waislamu wote nchini wataungana na waislamu wengine duniani ili kusherehekea siku hiyo ambayo itapambwa na shughuli mbalimbali ikiwamo maandamano ya amani,” alisema Sheikh Alhad.

Kutokana na hali hiyo, amewaomba Watanzania wote bila ya kujali tofauti za dini, rangi au kabila, kuungana na waislamu ili kusherehekea siku hiyo kwa kudumisha amani, upendo, mshikamano na umoja, jambo ambalo linaweza kujenga taifa imara.

Sherehe hizo kitaifa zitafanyika mkoani Singida katika Kijiji cha Sheruhi ambako Mufti Abubakar Zuberi ataungana na waislamu wengine katika mkoa huo na maeneo jirani ili kusherehekea siku hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles