22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU ATETA NA BALOZI WA MALAWI

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Benedict Mashiba, ambapo amemtaka kuimarisha mahusiano baina ya nchi zote mbili.

Alikutana na Balozi Mashiba jana katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi.

Pia amemtaka kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususani katika sekta ya viwanda.

Alisema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii, pia amemtaka kuboresha biashara baina ya Tanzania na Malawi kwa kutumia meli mbili za mizigo za Mv Ruvuma na Mv Njombe alizozizindua hivi karibuni.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amemtaka Balozi Mashiba kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio nchini Malawi na kuwasisitiza kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia kuwaunganisha pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Balozi Mashiba alisema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Malawi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles