28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

AIRTEL, VETA WAZINDUA NAMBA MAALUMU YA VSOMO

 

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Elimu ya Ufundi Stadi Tanzania (Veta) kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel kupitia mradi wa Airtel Fursa, wamezindua namba maalumu zitakazowafanya wateja au wanafunzi wanaojiunga na huduma ya masomo kupitia maombi ya VSOMO kupata maelekezo kupitia namba hiyo.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi huo, Mkuu wa Kanda wa Chuo cha Veta, Habib Bukko, alisema namba hizo zitasaidia kuwa na suluhisho kwa wanafunzi wanaokwama na kutaka taarifa kwa wakati ambapo wataweza kupiga simu moja kwa moja.

“Veta lengo letu ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kushiriki vyema kiutendaji katika sera ya uchumi wa viwanda, Veta kupitia huduma tunayotoa kupitia VSOMO tumeshirikiana tena na Airtel kwa kuhakikisha kuwa masomo ya Vsomo yanawafikia wengi.

“Tunazindua namba hii 0699859573 na 0699859572 zitakazowawezesha wanafunzi wenye nia ya kutaka kusoma kupitia mfumo wa VSOMO kuweza kukamilisha malengo yao bila kikwazo chochote kwa kuuliza na kusaidiwa muda wowote tunapokuwa wazi,” alisema Bukko.

Naye Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa ambaye ndiye msimamizi wa mpango wa VSOMO, Mhandisi  Lucias Luteganya, alisema: “Namba hizo maalumu zitahudumia wanafunzi au yeyote atakayepiga ili kupata msaada wa Veta kwa siku zote saba za wiki kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

“Tumeona kuna umuhimu wa kuweka namba hii iweze kuwahudumia hasa kwa kipindi hiki ambacho mpango huu wa Vsomo unazidi kupanuka kwa kuongeza kozi nyingi kulingana na mahitaji,” alisema Luteganya.

Upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano, alisema Airtel inaendelea kujisikia fahari kufanikiwa kuongeza ubunifu katika huduma zao.

“Uzinduzi wa namba hizi maalumu ni suluhisho lingine lakuendelea kurahisisha upatikanaji wa elimu ya ufundi stadi ili tupate wataalamu wakutosha katika sekta mbalimbali, namba hizi zitapatikana siku zote za kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni ambapo kila simu itakayopigwa itakuwa na gharama ya shilingi 60 tu na mteja hatapangiwa muda wa kuongea na mtoa huduma hadi mwisho wa kuhudumiwa.

“Vile vile ili kupata maelezo ya kutosha mwanafunzi anaweza kutembelea kurasa zetu za mtandao ya kijamii pamoja na website ili kupata maelekezo ya VSOMO wakati wowote,” alisema Singano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles