27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

UCHUMI WA VIWANDA BILA WANAWAKE BADO-TGNP

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Lilian Lihundi, amesema Serikali haiwezi kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda kama hakutakuwa na ushirikishwaji wa wanawake na vijana kikamilifu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lilian alisema kutokana na sensa ya mwaka 2012 zaidi ya asilimia 51 ya Watanzania wote ni wanawake hivyo Serikali haipaswi kuacha kundi kubwa hili nyuma katika kuleta maendeleo.

“Kwa wakati tuliokuwa nao sasa hivi ambao watu ni rasilimali kubwa sana katika maendeleo na ukiwa na kundi ambalo ni zaidi ya asilimia 51 katika nchi yako, huwezi kuwaacha pembezoni kwani ni lazima washiriki kikamilifu ili maendeleo yatokee.

“Kwa hiyo suala la usawa wa kijinsia, kushirikisha wanawake, vijana na makundi mengine ya watu wenye ulemavu katika mikakati ya maendeleo na kutenga rasilimali za kutosha ni suala la kimaendeleo hivyo kama tunahitaji twende haraka kimaendeleo, hili kundi la wanawake na vijana lisiachwe pembeni lazima lishiriki kikamilifu,” alisema Lilian.

Alisema inaweza kuchukua muda mrefu kufikia uchumi wa kati na wa viwanda kama makundi hayo hayatapewa nafasi na kuandaliwa mikakati mizuri kushiriki hivyo alitoa wito kwa Watanzania kuanzia ngazi ya kifamilia hadi kitaifa kutambua kuwa suala la usawa wa kijinsia ni la kimaendeleo.

Alisema pamoja na juhudi mbalimbali ambazo mtandao umekuwa ukizifanya kuhakikisha usawa wa kijinsia bado kuna changamoto ambazo wanakabiliana nazo likiwamo suala la ufinyu wa bajeti yenye mlengo wa kijinsia.

“Bado hatujafikia bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo inahakikisha kwamba makundi mbalimbali hususani wanawake na watu wenye ulemavu yanatengewa rasilimali za kutosha kulingana na mikataba ya kimataifa ambayo nchi imeiridhia

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles