24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU ASITISHA UJENZI HALMASHAURI TARIME

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesitisha uamuzi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime katika eneo la Nyamwaga baada ya kubaini hatua hiyo katika inaweza kuisababishia halmashauri kutumia fedha nyingi kwa ajili ya ulipaji wa fidia.

Waziri Mkuu ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Januari 17, mjini Tarime mkoani Mara wakati akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na Mji wa Tarime.

Amesema mbali na fedha nyingi zinazoweza kutumika kwa ajili ya fidia ya eneo hilo, lakini pia uteuzi wa eneo hilo haukufuata utaratibu na kushindwa kuzingatia jiografia ya halmashauri hiyo katika kuwasogezea wananchi huduma karibu na maeneo yao.

“Naagiza kusitishwa kwa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na wataalamu watakuja hapa hili kulifanya jambo hili kwa utaratibu unaofaa, serikali itatuma watalaamu katika Halmashauri ya Tarime vijijini ili kuangalia maeneo hayo kisha kutoa ushauri kwa eneo linalostahili kujengwa makao makuu hayo.

“Kumekuwapo na taarifa za kuibuka Kwa migogoro ya wapi pa kujengwa makao makuu na serikali haiwezi kukubali kuona migogoro inaibuka kutokana na suala la ujenzi wa eneo la Makao Makuu ya Wilaya,” amesema Majaliwa.

Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu amesema uamuzi huo ameufanya kama alivyofanya hivi karibuni wilayani Mbinga na kudai taratibu lazima zizingatiwe yanapofanyika masuala muhimu ya kuihudumia jamii.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles