HATMA YA WENYE VYETI FEKI KUJULIKANA MEI MOSI

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema hatima ya watumishi waliokuwa na vyeti feki kulipwa au kutolipwa itajulikana kabla ya sherehe za Mei Mosi mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TUCTA, Dk. Yahya Msigwa amesema hayo leo Jumatano Januari 17 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema wiki iliyopita walikuwa na kikao na mawaziri husika ambapo walielezwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na majibu yatajulikana kabla ya Machi au Aprili mwaka huu.

“Tumeambiwa kwamba mamlaka mbalimbali zinalifanyia kazi suala hili lakini bado tunaendelea kuipigia magoti serikali ufanyike ubinadamu ili hawa watu wasitoke mikono mitupu,” amesema Dk. Msigwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here