24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

KAMATI YA PROF KABUDI YAANZA MAZUNGUMZO NA TANZANITE ONE

Kamati ya kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite iliyoundwa na Rais John Magufuli imeanza kufanya mazungumzo na Kampuni ya Tanzanite One.

Kamati hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi imeanza mazungumzo hayo jana Jumanne Januari 16 kwa lengo la kuhakikisha nchi inanufaika na madini hayo yanayochimbwa Tanzania  pekee.

Profesa Kabudi amesema mazungumzo hayo yameanza vizuri huku pande zote mbili zikipitia matatizo yanayohusu biashara ya amadini hayo, utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za madini na mapato ya rasilimali hiyo ili hatimaye zikubaliane namna bora itakayohakikisha Tanzania inanufaika ipasavyo.

Mkurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Shabhai amesema kampuni yake iko tayari kwa majadiliano hayo inaunga mkono juhudi za kuhakikisha madini hayo yanainufaisha Tanzania tofauti na sasa ambapo inanufaisha nchi nyingine ambazo hazizalishi madini hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles