23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AMPA SIKU 15 MWEKA HAZINA SIKONGE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempa siku 15 Mweka Hazina wa Wilaya ya Sikonge, Evans Shemdoe kujieleza ni kwa nini ameshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya ndani.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo lhamisi, Agosti 10, wakati akizungumza na watumishi na watendaji wa wilaya hiyo, mjini Sikonge. 

“Nataka maelezo yakayoniridhisha ni kwa nini hamkufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya halmashauri ambacho ni kiwango cha chini. Nzega wamefikisha asilimia 112, Kaliua wana asilimia 91, Nzega wana asilimia 80, ni kwa nini wewe umeshindwa kufikisha kiwango hicho?

“Ninataka nipate maelezo pia ni ipi mipango yenu ya kukusanya mapato kwa maeneo mliyoshindwa kufanya vizuri, na pia mmejipangaje kwa mwaka ujao wa fedha. Niyapate maelezo hayo ifikapo Agosti 25,” amesema.

Akijibu kuhusu kushindwa kukusanya mapato hayo kwa asilimia 80, Shemdoe amesema wamefikisha asilimia 76.7 na wameshindwa kufikia lengo kwa sababu ya upungufu wa mvua katika msimu uliopita, hali ambayo ilichangia kushuka kwa mavuno ya zao la tumbaku miongoni mwa wakulima.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles