24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

ALEXIS SANCHEZ NJE YA UWANJA WIKI MBILI

LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez, ataikosa michezo miwili ya awali ya Ligi Kuu nchini England kutokana na kusumbuliwa na tumbo mazoezini.

Mchezaji huyo ambaye anashinikiza kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho katika kipindi hiki cha majira ya joto, ataukosa mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Leicester City kesho Ijamaa na Jumamosi ya wiki ijayo dhidi ya Stoke City.

Hata hivyo, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amewaondoa wasiwasi mashabiki wao kwamba mchezaji huyo atajiunga na wenzake baada ya hali yake kuwa sawa na kukitumikia kikosi chake.

Wenger aliongeza kwa kusema tayari wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo juu ya kumwongezea mkataba mpya, hivyo wamefikia pazuri na kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza mkataba mpya.

“Katika michezo yetu miwili ya mwanzo katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, tutamkosa mshambuliaji wetu, Sanchez.

“Mchezaji huyo amepatwa na tatizo kidogo la tumbo wakati wa mazoezi ya mwisho, hivyo anatakiwa kufanyiwa vipimo ili kuangalia tatizo alilonalo, kuna uwezekano mkubwa wa kuikosa huduma ya mchezaji huyo kwa wiki mbili,” alisema Wenger.

Katika suala la kumwongezea mkataba, Wenger alisema kila kitu kupo wazi na kuna uwezekano wa kumalizana na mchezaji huyo hivi karibuni.

“Kuna uwezekano mkubwa wa kumwongezea mkataba mpya, siku zote mchezaji akiwa anafikia mwisho wa mkataba wake tunakuwa na mazungumzo naye juu ya kumwongezea, hatuna sababu ya kumuacha Sanchez akiondoka, tupo kwenye hatua za mwisho sasa,” aliongeza Wenger.

Hata hivyo, kocha huyo ameweka wazi kuwa hadi sasa hajapokea ofa yoyote kutoka kwa klabu ya PSG na nyingine ambazo zinadaiwa kuonesha nia ya kuitaka saini ya mchezaji huyo.

“Hadi sasa sijafanya mazungumzo yoyote na mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, juu ya kutaka kumsajili Sanchez, alikuwa anapambana kuhakikisha anaipata saini ya mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, nadhani kwa sasa wanaifuatilia saini ya Kylian Mbappe na wala si Sanchez.

“Kwa sasa siangalii juu ya kupokea ofa kwa kuwa nilishasema tangu awali kuwa mchezaji huyo hauzwi, bado Arsenal inahitaji huduma yake hadi pale mwisho wa mkataba wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles