22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

REAL MADRID MABINGWA UEFA SUPER CUP

 

SKOPJE,JAMHURI YA MACEDONIA

MABINGWA wa Ligi Kuu nchini Hispania na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, wamefanikiwa kutwaa Kombe la UEFA Super Cup baada ya kuwachapa wapinzani wao, Manchester United mabao 2-1 juzi mjini Skopje.

Madrid walionekana kuutawala mchezo huo kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo, huku wachezaji wake, Casemiro na Isco, wakiibeba timu hiyo kwa kufunga bao moja moja na bao la Manchester United likifungwa na Romelu Lukaku, lakini United walishindwa kutumia nafasi ya wazi aliyoipata mchezaji wao, Marcus Rashford, aliyejikuta akiutoa mpira nje.

Real Madrid wameweka historia ya aina yake ya kuwa klabu ya kwanza kufanikiwa kutetea Kombe la UEFA Super Cup, huku mara ya mwisho kombe hilo likitetewa mwaka 1990.

Mchezo huo wa juzi ulipigwa uwanja wenye joto kufikia nyuzi 30, kwenye mji mkuu wa Macedonia. Wachezaji walipewa muda mara mbili wa kwenda kunywa maji kwa ajili ya kupoza joto ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Uefa.

Mbali na Manchester United kufanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha majira ya joto, lakini bado walionekana kuwa na wakati mgumu dhidi ya wapinzani wao Real Madrid.

Manchester United kipindi hiki cha usajili imetumia kiasi cha pauni milioni 146 kununua wachezaji watatu ambao ni mshambuliaji wa Everton, Lukaku kwa pauni milioni 75, kiungo wa kati wa Chelsea, Nemanja Matic, kwa pauni milioni 40 na beki wa Benfica, Victor Lindelof, kwa pauni milioni 31.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho, alitangaza kuwa kwenye mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa Real Madrid, Gareth Bale, lakini amethibitisha kuwa mipango hiyo itakuwa migumu kutokana na rais wa Madrid, Florentino Perez, kudai bado wanahitaji huduma ya mchezaji huyo ambaye alionesha kiwango kizuri kwenye fainali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles