27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu afikisha ujumbe wa Rais Samia Stars

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ana matumaini makubwa na timu ya Taifa, Taifa Stars na anaamini itafanya vizuri na kufuzu kushiriki Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 5, 2021, wakati alipozungumza na wachezaji wa Taifa Stars kambini kwenye hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kutoa hamasa kuelekeza mchezo na DR Congo, Novemba 11,2021 kwenye Uwanja wa Mkapa na Madagascar Novemba 14,2021.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Nahodha wa timu ya Taifa Stars, John Bocco  kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jjjini Dar es salaam Novemba 5, 2021 alikokwenda kutoa hamasa  kwa timu hiyo   kuelekea mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya timu ya Taifa ya Congo na Madagascar.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wataendelea kuisimamia na kufuatilia maendeleo ya timu hiyo hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha inafanya vizuri.

“Mheshimiwa Rais ana matumaini makubwa na nyinyi na anawatakia kila la kheri katika maandalizi yenu, ni matumaini yake kuwa mtafanya vyema na kufuzu hatua ya kumi bora na hatimaye kupata nafasi kuwa miongoni mwa timu tano zitakazo shiriki kombe la Dunia kutoka Afrika.

Waziri Mkuu amewasihi wachezaji  hao kujitoa na kufanya mazoezi kwa bidii, pamoja na kuzingatia maelekezo wa mwalimu na wataalam wa benchi la ufundi ili kuhakikisha ushindi unapatikana.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wachezaji wa Taifa Stars ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya timu ya Taifa ya Congo na Madagascar katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam

“Viongozi wa kamati ya hamasa ya Taifa Stars kwa kushirikiana na TFF hakikisheni mnaisimamia timu vyema, wachezaji wale vizuri na wafanye mazoezi na wapewe kila kinachohitajika ili kujihakikishia tunapata ushindi,”amesema Majaliwa.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Taifa Stars, John Bocco ameahidi kuwa watajitoa kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi zote zilizobaki.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi  kutoka TFF wakiongozwa na Katibu Mkuu Wilfred Kidau, viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars, Ghalib Mohamed na Makamu Mwenyekiti Salim Abdala “Try Again” na Katibu wa Kamati hiyo Hersi Said.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles