25.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Makamba: Wizara itasimamia miradi ya umeme nchini

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema wizara yake itasimamia miradi ya umeme na gesi asilia ili kuweza kupatikana kwa umeme wa uhakika.

Makamba maeyasema hayo Julai 6, 2022 baanda ya kutembelea Mabanda katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) ndio kitovu kinachotegemewa kwa kiasi kikubwa katika uendeshaji wa shughuli za uchumi.

“Kaulimbiu ya mwaka huu inasema Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji na sisi kama shirika tutahakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika ili kuweza kuendesha shughuli za kiuchumi,” amesema Makamba.

Ameongeza kuwa ushiriki wa taasisi za umma katika maonyesho hayo ni kusogeza huduma karibu kwa wananchi.

Amesema wananchi wakitembelea banda la REA, TPDC na TANESCO watapata elimu, huduma pia wataweza kuona kazi nzuri zinazofanywa na mashirika hayo.

Amesema Tanesco ni shirika ambalo limekuwa likifanya mabadiliko kila mwaka katika kushiriki maonyesho hayo.

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mharage Chande amesema shirika hilo lina miradi mingi ambayo inalisimamia japo kwasasa mradi wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ndio mradi wa kimkakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles