24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania jitokezeni kuchangia Mwitikio wa UKIMWI – Kigaigai

*Awatahadharisha kujikinga na maambukizi ya VVU

Na Nadhifa Omary, Kilimanjaro

Wananchi mkoani Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kuchangia mwitikio wa UKIMWI huku wakiaswa pia kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kwakuwa mwenye maambukizi huwezi kumjua kwa macho.

Hayo yamebainishwa na Julai 5, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake juu ya uhamasishaji wananchi kushiriki zoezi la Kili Challange linalohusu upandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai(kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko wakati akisisitizia umuhimu wa Watanzania kushiriki katika kuchangia fedha katika Mwitikio wa UKIMWI nchini, wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Waandishi wa Habari Julai 5, 2022 kuhusu upandaji wa Mlima Kilimanjaro kupitia kampeini ya Kilichallange inayoandaliwa na GGML kwa ushirikiano wa TACAIDS.

Kigaigai amesema kwa mujibu wa Takwimu za Kitaifa zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa mwaka, Tanzania kuna maambukizi 68,000 kwa mwaka sio kidogo na wala huwezi kutambua kati ya hao 68,000 nani ana maambukizi au nani hana.

“Nawaomba wana Kilimanjaro tujikinge na maambukizi ya VVU,tumemsikia Mkurugenzi wa TACAIDS hapa anasema maambukizi kwa sasa yapo 68,000 kwa mwaka, kinachosadia kwa sasa ni hizi ARV ambazo watu wanazitumia na wanapendeza, mwenye VVU huwezi kumtambua kwa macho kikubwa tujikinge wenyewe,” amesema Kigaigai.

Akifafanua kuhusu Kili Challenge against HIV and AIDS amesema ni harambee ya uchangiaji wa fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI ukilenga zaidi jamii zilizoko kwenye mazingira hatarishi ya maambukizi ya VVU na kupunguza athari za UKIMWI.

Amefafanua kuwa kwa mwaka huu zoezi hilo litazinduliwa mkoani Kilimanjaro Julai 14, 2022 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene.

Kwa mujibu wa ratiba ya mbio hizo, Julai 15, mwaka huu wapanda mlima na waendesha baiskeli watapanda mlima Kilimanjaro kupitia lango la Machame ambalo ndio njia yenye changamoto kubwa iliyopendekezwa mahususi kuonesha jinsi mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI yalivyo na changamoto.

Aidha, Julai 21, wapanda mlima hao watapokelewa katika lango la Mweka na mgeni rasmi katika siku hiyo atakuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai.

Amezitaja huduma zitakazotolewa wakati wa zoezi hilo kuwa ni elimu ya kujikinga maambukizi ya VVU, Upimaji wa VVU, chanjo ya Uviko-19 na uchangiaji wa damu, amewataka wananchi kujitokeza kupata huduma hizo kwani zitakuwa zikitolewa bila malipo.

Tukio hili hufanyika kila mwaka chini ya uratibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML) ambapo limeanza tangu mwaka 2002 na hadi kufikia sasa takribani zaidi ya dola milioni 7 zimekusanywa na kugaiwa kwa walengwa.

Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amesema jitihada za Kili Challenge zinalenga kuziba pengo la wafadhili wa fedha za UKIMWI ambao wamekuwa wanapungua kila mwaka wakati mahitaji ya fedha za mwitikio wa UKIMWI bado ni makubwa.

“Wafadhili katika mwitikio wa UKIMWI wanapungua kila mwaka lakini mahitaji ya fedha za UKIMWI ni makubwa, hivyo nawaomba Watanzania wajitokeze kuchangia Mwitikio wa UKIMWI kwa kadri wanavyoweza kwa kutumia njia ya kili challenge au kupitia Mfuko wa udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF), pia iwapo mtu au Kampuni ipo tayari aje tuone namna tutakavyojipanga tukaanzisha njia nyingine tofauti na hizi mbili,” amesema Maboko.

Aidha, Dk. Maboko amefafanua kuwa sasa hivi serikali tayari imefanya marekebisho katika sheria ya kodi kwa Kampuni, taasisi au shirika litakalo changia katika mfuko wa ATF ule mchango wake wote utapungzwa katika makato ya kodi ya mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles