25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Bashungwa azindua filamu ya maisha ya hayati Dk. Magufuli

Na Brighiter Masaki, Dar es salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa jana April 8 amezindua filamu ya Hayati Dk. Magufuli na kuikabithi Makumbusho ya Taifa.

Filamu hiyo inayoonyesha enzi za uhai wa hayati magufuli hadi kifo chake pamoja na kumbukumbu nyingine ilikabidhiwa makumbusho ya Taifa kama moja ya kumbukumbu kwa Watanzania.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ya filamu usiku wa kuamkia leo, Bashungwa amewataka wasanii kuungana kuwa kitu kimoja na wakikutana wanatakiwa kupanga mikakati ya maboresho ya tasnia na sio kusuluhisha migogoro.

“Nimefurahi kuona wasanii wamefanya kitu ambacho kitakuwa ni kumbukumbu ya kumuenzi aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Dk. Magufuli.

“Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi na Hayati Magufuli kwa kuwa aliamini katika kujenga na kuwataarisha vijana kwa maisha ya baadaye,” amesema Bashungwa

Aidha amesema kuwa Hayati Magufuli amewafundisha nini maana ya kazi, pia atamzungumzia kwa mazuri aliyoyafanya wakati wa enzi za uhai wake katika madaraka ya kuiongoz nchi ya Tanzania.

“Amefanya mambo makubwa ambayo Afrika na Dunia inashangaa amekuwa Rais kwa muda mchache lakini amefanya mambo makubwa, maisha yake yanatuonyesha vijana tuna uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa muda mchache.

“Nawapongeza wasanii kwa kutengeneza filamu hiyo na hayati magufuli alikuwa anapenda sanaa, ameniachia deni la kuwapenda na kuamini kwamba COSOTA ni chombo ambacho kinahitaji kuimarishwa kwa hivyo wasanii wasijione wako peke yao,” amesema Bashungwa

Pia ameongeza kuwa “Nitatafuta muda nikutane na wadau wa filamu na kusikiliza changamoto zao huku tukirekebisha sheria ili ifikapo julai wasanii wanufaike na kazi zao kutokana na mifumo tunayoindaa, pia natoa wito kwa wasanii kujisajiri kupitia vyama vyao ili iwe rahisi kuwafikia”.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt Kiagho Kilonzo, amesema hayati Dk. Magufuli alikuwa mtetezi wa wasanii hivyo wasanii wa filamu Pamoja wakishirikiana na uongozi wametengeneza filamu ambayo itakuwa kumbukumbu ya maisha yake hapa Duniani.

“Katika uhai wake alikuwa metetezi wa wasanii hivyo kutokana na pigo la kuondokewa naye tumeona tumuenzi kwa kutengeneza filamu hiyo ambayo itakuwa kumbukumbu ya maisha yake.

“Filamu hii imeandaliwa na wasanii kwa kujitolea kwa maana mwenye camera alijitolea mwenye kuigiza alijitolea na wote walioshiriki walijitolea kwa maana hiyo wasanii wamejitolea ili kurudisha fadhira kwa Watanzania na Serikali yetu ili kumuenzi”, amesema Kilonzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles