27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

IGP Sirro atoa agizo la operesheni ya madawa ya kulevya

Na Brighiter Masaki, Zanzibar

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda IGP Simon Sirro, amewataka Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Tanga, visiwani zanzibar kufanya operesheni ya pamoja kudhibiti makosa ya dawa za kulevya.

IGP Sirro ametoa maagizo hayo leo Aprili 8 akiwa kisiwani Zanzibar ambapo amesema katika kipindi cha miezi mitatu makosa ya jinai yamepungua kwa asilimia 19.1 huku makosa ya usalama barabarani yakipungua kwa asilimia 14.

“Bado madawa ya kulevya ni shida lakini makamanda wa mkoa wa Mtwara, Lindi, Tanga, Dar es Salaam na makamanda wote wa visiwani zanzibar ni lazima wafanye operesheni za pamoja hili suala haliwezi kutushinda ikiwa uwezo mkubwa tunao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama” amesema IGP Sirro.

Pia IGP Sirro amendelea kusisitiza kwa viongozi wa dini kushirikiana na polisi ili kukabiliana na suala la matukio ya udhalilishaji wa kijinsia.

“Bado makosa ya uzalilishaji wa kijinsia ni mtambuka na sheria ni msumeno wewe Sheikh ukifanya kosa sheria ichukue mkondo wake, na Padri akifanya kosa sheria ichukue mkondo wake lakini ni msingi sana watu wabadilishe fikra zao,” amesema IGP Sirro

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles