24.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Bashe azindua kituo atamizi cha Mkonge BBT

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Tanga

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), kuweka utaratibu mzuri kuhakikisha kunakuwa na vifaa vyote muhimu katika Kituo Atamizi cha Mkonge BBT kilichopo Tanga.

Waziri Bashe ameyasema hayo baada ya kuzindua kituo hicho kinacholenga kutoa mafunzo ya ubunifu na uzalishaji wa bidhaa za mkono zitokanazo na singa za mkonge, uzalishaji nzi chuma, utengenezaji wa karatasi, mafunzo ya ukataji na uchakataji Mkonge.

Amesema kituo hicho kinahitaji kuwa na vifaa ili kina mama, wenye ulemavu na vijana wanaozalisha bidhaa mbalimbali wakija wakute vifaa vyote muhimu ambapo pia
watatumia kituo hicho kama sehemu ya kuzalishia mali kisha kwenda kufanya biashara zao nje.

“Naagiza tupate vifaa vyote muhimu ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kufanya shughuli ndogondogo za uzalishaji mkonge ili vikundi vya wajasiriamali kina mama na vijana wakipata mkopo wa asilimia 10 wa halmashauri, wana uwezo wa kwenda kununua singa za mkonge au malighafi hawahitaji kununua mashine, watazikuta hapa.

“Mkonge ni zao muhimu katika uchumi wa nchi, zipo bidhaa nyingi zinazotokana na konge. Bodi imeingia makubaliano na wenzetu ambao wamekuwa wakifundisha namna ya kutumia mabaki ya mkonge katika kuzalisha karatasi,” amesema,” amesema Bashe.

Waziri Bashe amesema Serikali imeweka dhamira kupitia maombi ya bodi takribani Sh milioni 600 kwa ajili ya kuweka Kituo Atamizi Tanga na Zanzibar ambapo Tanga itakuwa kituo ambacho vitawekwa vifaa vyote vidogovidogo vya kuongeza thamani mkonge na mazao mengine madogo madogo ya kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mkonge wa TSB, Olivo Mtung’e, amesema kituo hicho kimeanzishwa Tanga kwa sababu mkonge unalimwa zaidi na ndiyo makao makuu ya TSB.

Amesema kituo hicho Atamizi lengo lake ni kuwawezesha vijana, wanawake na wenye ulemavu kujiajiri, pia watakwenda kuwasaidia ambao wanazalisha mkonge hasa kwa upande wa Tanga ambao walikuwa wanakosa soko la kuuza mkonge nje.

“Soko letu bado linategemea zaidi kuuza nje huku ndani matumizi siyo makubwa sana
lakini tunatambua kuwa vijana wetu, kina mama hawana ajira za kuwaingizia kipato kwa hiyo tunategemea kituo hiki kuwa na watu ambao watajiajiri. Pia tutaongeza matumizi ya zao la mkonge kwa upande wa ndani.

“Lakini pia kituo hiki ni sehemu ya kwanza tu kuna vituo vingi vinakuja kutakuwa na mashine ya kutengeneza bidhaa za mkono za kufuma kama vile kamba na cha pili kinaratajiwa kuanzishwa hapa hapa Tanga kwa ajili ya kutengeneza karatasi na gypsum na vitu vya kuezekea,” amesema Olivo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles