Waziri Aweso awakutanisha Dawasa na wabunge wa Dar na Pwani

0
250

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso leo Jumatano Desemba 30, amefungua kikao kazi cha siku moja kati ya Menejiment ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) na wabunge wa Mkoa wa Dar na Pwani.

Kikao hicho kinalenga kuimarisha mahusiano na kutatua changamoto za upatikanaji huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo yao.

Aweso ametoa wito kwa DAWASA kufanya kazi kwa karibu na Wabunge pamoja na Wawakilishi wa wananchi ili kujenga uelewa mpana wa mipango mbalimbali iliyopo ya kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi wa Dar es salaam na Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here