24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CMSA yaidhinisha hamisho la hisa za Rabobank katika Benki ya NMB

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeidhinisha uhamisho wa hisa zinazomilikiwa na Rabobank ya Uholanzi katika Benki ya NMB kwenda Arise B.V. (‘Arise).

Taarifa iliyotolewa na beki hiyo leo Desemba 30, imefafanua kuwa, Arise B.V., ambalo ni jukwaa la uwekezaji, ni kampuni ya Kiafrika ya uwekezaji inayoongoza na kufadhiliwa na wawekezaji mahili.

Aidha imesema kuwa, muungano wa wawekezaji hao ulianzishwa mwaka 2016 na Mfuko wa Taifa wa Maendelro wa Norway (Norfund), Benki ya Maendeleo ya Uholanzi (FMO) pamoja na kampuni ya huduma za kifedha ya kimataifa ya Uholanzi – Rabobank.

Hivyo, hiyo ina maana kwamba, Rabobank bado ni sehemu ya wamiliki/umiliki wa NMB Bank Plc kupitia Arise.

Lengo la Arise ni kuziendeleza taasisi za ndani za fedha na masoko yenye uwezo mkubwa wa kukua, NMB na Tanzania zikiwa miongoni mwa maeneo pendwa ya kiuwekezaji katika nchi za Afrika zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara (SSA) la kampuni hiyo.

Kuidhinishwa kwa hamisho la hisa za Rabobank ndani ya Benki ya NMB kutapelekea hisa 174,500,000 ambazo ni sawasawa na asilimia 34.9 ya hisa zote za benki hiyo, kuhamishiwa Arise.

Idhinisho la CMSA linakuja baada ya ombi la hamisho la hisa la Rabobank kupata baraka kutoka mamlaka zote husika za kiudhibiti.

Akiongea kuhusu hamisho hilo la hisa, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema kuwa; “Kufanikiwa kukamilika kwa hamisho la hisa ni ushuhuda tosha wa imani ya wawekezaji katika taasisi yetu na nchi kwa ujumla.

“Ushirikiano kati ya Arise na NMB unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kiutendaji, kibiashara, kimuundo na kifedha ukiwa na tija ya muda mrefu kimasoko ambayo itazidi matarajio ya wanahisa,” amesema Ruth.

Ikumbukwe kuwa NMB ni benki kubwa Tanzania kirasilimali kwa mujibu wa matokeo ya shughuli za kifedha za robo ya tatu ya mwaka huu. Rasilimali zake ziliongezeka kwa kuweka rekodi hadi Sh trilioni 7.0 kutoka Sh trilioni 6.1 kipindi kama hicho mwaka 2019.

Pia, NMB ni benki inayoongoza kwa kutengeneza faida, baada ya kuwa imepata Sh bilioni 145 wakati wa robo ya mwaka iliyoishia Septemba 30, 2020, hili likiwa ni ongezeko la Sh bilioni 82 mwaka 2019.

“Bila shaka uwekezaji huu wa muda mrefu wa Arise utasaidia matarajio ya ukuaji wa siku za usoni wa NMB na kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa Tanzania kupitia ongezeko la huduma jumuishi za kifedha, na ukuaji wa sector za biashara ndogo ndogo, kampuni za kijasiriamali na kilimo.

“Benki ya NMB inapenda kuwashukuru wanahisa wote, washirika wa kimkakati, wateja na wafanyakazi wake kwa kuendelea kuiamini na kuidhamini,” amesema Ruth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles