Waziri ataka walioua mbwa mwitu wasakwe

0
1342

wild-dogs-on-road

Na JANETH MUSHI, ARUSHA

VYOMBO vya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA),vimeagizwa kufanya uchunguzi ili kuwabaini, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa waliohusika na mauaji ya mbwa mwitu 11 wilayani humo.

Hivi karibuni iliripotiwa kuuawa kwa mbwa mwitu hao ambao walipewa sumu na watu wasiojulikana.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Chakula Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha, alipokuwa akizungumza katika  kuwasimika viongozi wapya wa mila ya kimasai katika Kata ya Nainokanoka wilayani humo.

Ole Nasha ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro, alisema tukio la kuuawa kwa mbwa mwitu hao kumezua wasiwasi kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo, kwani kwa kipindi kirefu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here