27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ataka kambi ya kudumu

kigwangal3NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, DK. Hamis Kigwangala, ameipa miezi sita Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kujenga kambi ya kudumu ya wagonjwa wa Kipundupindu.

Agizo hilo la Dk. Kigwangala linakwenda kinyume na mtazamo wa Rais Dk. John Magufuli ambaye amekuwa akihimiza suala la usafi ili kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini.

Katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa, Rais Magufuli alifuta sherehe za Uhuru za Desemba 9, mkwaka huu na kutaka watu watumie siku hiyo kwa kufanya usafi ili kutokomeza ugonjwa huo.

Jana Dk Kigwangala, alimpa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi na watendaji wake miezi sita, kuhakikisha wanajenga kambi ya kudumu ya wagonjwa hao baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo
cha Afya Buguruni kwa Mnyamani.

“Siridhishwi na mazingira ya kambi ya kipindupindu kwani ipo jirani na makazi ya watu, pia ni hatari hata kwa
wagonjwa wanaokuja kupata tiba katika kituo hiki,”alisema Dk.Kigwangala.

Alisema ili kufanya maboresho ni vyema mkurugenzi akatafuta eneo jingine ambako kambi hiyo itajengwa.
Pia waziri huyo alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchi nzima kuhakikisha wanatengeneza mpango kazi
wa kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kufanya usafi.

“Nataka ndani ya siku tatu niwe nimepata mpango huo jinsi utakavyo tekelezwa,,”alisema. Naye Nyakongo Manyama wa Idara ya Habari Maelezo, anaripoti kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kwa wastani ugonjwa wa kipindupindu umepungua katika mkoa wa Dar es salaam na kwa mikoa ya Iringa na Moshi kwa kiasi kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles