26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Ikulu yamsimamisha mkurugenzi K’ndoni

DSC_0092NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jumanne Sagini amemsimamisha
kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, Mhandisi Mussa Natty ili asubiri uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Natty kuhamishiwa Babati mkoani Manyara kabla ya kurejeshwa Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilifafanua kuwa pamoja na kusimamishwa kazi, Mhandisi Natty anapaswa kurudi katika Manispaa ya Kinondoni kusubiri uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Taarifa hiyo ilitaja tuhuma zinazomkabili kuwa ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za manispaa
ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango na kutowachukulia hatua watendaji wa manispaa waliokua chini
yake.

Tuhuma nyingine ni ukosefu wa uadilifu katika ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa Coco na malalamiko ya wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni ulioambatana na usimamizi duni wa watumishi hasa wa sekta ya mipango miji na ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles