26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

MRI, CT-Scan zaharibika tena Muhimbili

mri--1NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MASHINE ya MRI na CT-Scan zilizoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zimeharibika tena, licha ya kufanyiwa matengenezo siku kadhaa zilizopita baada ya Rais Dk. John Magufuli kuamuru zitengenezwe haraka.

Hii ni mara ya tatu sasa tangu mashine hizo zilipoanza kuharibika mapema mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.
R a i s Magufuli alitoa amri ya kutengenezwa kwa m a s h i n e hizo Novemba 9, mwaka huu alipofanya ziara ya
kushtukiza hospitalini hapo, siku nne tangu alipoapishwa kuwa  rais.

K a t i k a ziara hiyo, Rais Magufuli alikuta mashine hizo zikiwa zimeharibika na kukuta idadi kubwa ya wagonjwa
wakisubiri huduma bila mafanikio.

Baada ya matengenezo hayo, mashine hizo zilifanya kazi kwa muda wa siku mbili na kuharibika tena Novemba
25 na kuanza kufanya kazi Novemba 26 baada ya kutengenezwa na Kampuni ya Philips, hadi sasa zilipoharibika tena.

Akizungumza hospitalini hapo jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema uongozi wa hospitali hiyo umemweleza kwamba mashine hizo zimeharibika tangu juzi.

Alisema kuharibika kwa mashine hizo kutokana na mashine hizo kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu, tangu zilipoanza kufanya kazi hospitalini hapo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence Mseru alisema watakaa na wadau ili kuona namna ya
kuwasaidia wagonjwa watakaokuwa wakihitaji huduma ya vipimo hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles