24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI AHIMIZA WANANCHI KULIPIA UPIMAJI ARDHI

Na SHEILA KATIKULA-MWANZA

NAIBU Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, amewataka wananchi kulipia gharama za upimaji wa viwanja katika zoezi linaloendelea kufanyika nchi nzima.

Mabula alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyamanoro Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Alisema wananchi wanapaswa kuchangia kwa kulipia gharama ya zoezi la upimaji shirikishi ambayo ni Sh 150,000 na kubainisha kuwa kufanya hivyo kutaliwezesha zoezi hilo kwenda kasi ili nao wapate hati za umilikaji ardhi.

“Nimeambiwa kuna watu wanagoma kulipa, hakikisheni mnalipa. Gharama ni Sh 150,000 na ukimaliza hapo unangoja kupewa hati, sasa huwezi kupewa kama hujakamilisha lakini kwa wale ambao hali imewabana kidogo wanaweza kulipa kidogo kidogo,” alisema.

Alisema zoezi hilo linapaswa kufanyika mapema kabla ya kukamilika kwa ‘Master Plan’ na kwamba itakapokuwa tayari iwe ni wakati ambao kila mmoja anamiliki hati yake.

Mabula alisema serikali iliamua kuja na mkakati wa urasimishaji makazi baada ya kuona kasi ya wananchi kujenga ni kubwa kuliko kasi ya wataalamu kupima maeneo na hatimaye kujenga bila utaratibu hali ambayo ilikuwa ikiifanya miji kutokuwa katika mpangilio mzuri.

Aliwataka wenyeviti wa Kamati za Urasimishaji makazi kuhakikisha migogoro yote inayojitokeza wakati wa zoezi hilo inatatuliwa sambamba na kuyatambua maeneo kwa kuyawekea bikoni.

Alisema mara baada ya upimaji huo na mpango mji (master plan) kuzinduliwa, wananchi watatakiwa kuomba kibali kwa ajili ya kujenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles