27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

HAKI ZA BINADAMU: SERIKALI ITOE TAMKO SHAMBULIO IMMMA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeitaka serikali kutoa tamko kukemea tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa Ofisi ya Mawakili ya IMMMA Advocates, lililotokea Agosti 26, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 29, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Helen Kidjo-Bisimba amesema kinalaani tukio hilo na kinasikitika tangu kutokea kwa tukio hilo serikali haijatoa tamko isipokuwa utetezi wa polisi wakijitetea kuhusu sare walizovaa watu waliovamia na kulipua ofisi hiyo.

“Viongozi wa serikali na vyombo vyake vyenye dhamana ya kulinda usalama wa watu nchini na haki za binadamu kwa ujumla wawajibike au kuwajibishwa mara moja pale ambapo wameshindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao, tunasikitika hadi leo hii hatujasikia kauli ya serikali kulaani kitendo hiki.

“Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaitaka serikali kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha wahusika wa shambulio la Ofisi ya IMMMA Advocates wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria haraka iwezekanavyo,” amesema Bisimba.

Pamoja na mambo mengine amesema wanaunga mkono mgomo wa siku mbili wa mawakili lakini pia ametaka tasnia ya sheria iachwe huru katika kufanya kazi zake na kupatiwa ulinzi kwa mujibu wa sheria na wanasheria waachwe watekeleze majukumu yao bila kuingiliwa au kutishwa.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu alisema hawatawafanya chochote mawakili watakaokwenda mahakamani katika siku mbili walizoangaza za mgomo isipokuwa watakuwa wameunga mkono utawala wa mabomu na wajijue hawako salama.

“Hili jambo lipigiwe kelele, hizi si siasa, tumetunga sheria miaka mitano inayosema kila mwenye kesi mahakamani anastahili kupata msaada wa kisheria mahakamani, sasa huo msaada mtaupata wapi kama wanasheria hatuko salama,” amehoji Lissu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles