31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

UHABA WA MAJI SAFI WAITESA MASWA

Na SAMWEL MWANGA -MASWA

MJI wa Maswa mkoani Simiyu umekumbwa na tatizo la uhaba wa maji safi kutokana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA) kusitisha uzalishaji kwenye bwawa la New Sola, baada kupungua kwa kina cha maji.

Akitoa taarifa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Merchades Anaclet, alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na kina cha maji kupungua na kufikia Sentimita 60.

Bwawa hilo, ambalo ndilo chanzo kikuu cha maji katika Mji wa Maswa pamoja na vijiji 11, linategemewa na wakazi wapatao 78,190 na mifugo zaidi ya 400,000.

Alisema kutokana na hali hiyo, mamlaka yake imeamua kuzima pampu za maji baada ya kufikia kina cha chini cha maji ambacho iwapo wataendelea kusambaza maji yote yatakuwa na mchanganyiko wa tope.

Alisema kuwa, kwa sasa mamlaka hiyo imewasiliana na Wizara ya Maji ili waweze kulichimba tena upya bwawa hilo kwa ajili ya kuondoa tope lililopo, ili kulirudisha katika hali yake wakati wakisubiria mvua zinyeshe.

“Tumeamua kuzima mitambo ya kusukuma maji katika chanzo chetu kikuu cha maji, kwani hali ya kina cha maji siyo nzuri, lakini wakati huo tunafanya mawasiliano na Wizara ya Maji ili tusaidiwe kuondoa tope lililojaa wakati tukisubiri mvua zinazotegemewa kuanza Oktoba, mwaka huu,” alisema.

Alisema kuwa, ili kukabiliana na hali hiyo, Mauwasa imepanga kutumia visima virefu vinne kuwasambazia maji kwa kutumia hadi hapo tatizo hilo litakapopatiwa ufumbuzi, hasa wakati wa mvua za masika.

Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk. Seif Shekalaghe, alisema hatua za dharura kwa ajili ya maji zinahitajika haraka ili kunusuru maisha ya watu.

Alisema moja ya sababu za bwawa hilo kukauka mapema ni kutopata mvua za kutosha katika msimu uliopita, huku akionya watu  wanaofanya shughuli za kibinadamu kandokando ya bwawa kuacha mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles