26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri aagiza wamiliki wa mashamba mgodi wa dhahabu Simiyu kupewa leseni

Na Derick Milton, Simiyu

Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya ameiagiza tume ya madini, kukipatia leseni kikundi cha wamiliki wa mashamba katika mgondi namba mbili wa Bulumbaka (Umoja Bulumbaka) uliko wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu ili kuondoa mgogoro uliopo sasa katika mgodi huo.

Prof. Manya ametoa maagizo hayo leo Jumatano, Januari 13, wakati akiongea na viongozi wa Wilaya, na Mkoa wakati wa ziara yake ambayo ilikuwa na lengo la kutatua mgogoro uliopo kwenye mgodi huo ambao unahusisha wamiliki wa mashamba.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa wamiliki hao wapewe leseni kwa ajili ya kusimamia mgodi huo kama ambavyo walitaka, huku akielekeza kuwa wapewe masharti yote wanayotakiwa kuzingatia kwenye leseni hiyo.

“Ili kumaliza mgogoro huo, ambao unaonekana shida kubwa ni hawa wamiliki, tuwapatie nao leseni kati ya zile ambazo ziliombwa, lakini wapewe wanatakiwa kuzingatia masharti yote yalipo kwenye leseni hiyo.

“Wakipewa hiyo leseni hasa kwenye mgodi wao huo namba mbili, waambiwe kuwa hawana mamlaka ya kuzuia watu wengine wafanye shughuli za uchimbaji, kwenye maeneo ambayo yanazunguka mgodi wao,” amesema Prof. Manya.

Naibu Waziri huyo amewataka vingozi hao pamoja na wachimbaji, kitambua kuwa sehemu yeyote ikitokea mlipuko wa madini, lazima iendelezwe kwa watu kupewa leseni ili kuweza kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Lazima mtambue kuwa rasi yeyote lazima iendelezwe kwa kupewa mtu, au kikundi kupewa leseni kwa ajili ya kundesha, faida yake ni kubwa kwani leseni inawajali watu wote wakiwemo wananchi, wamiliki wa mashamba na serikali,” amesema Prof. Manya

Awali akitoa taarifa ya mgogoro huo Afisa Madini Mkoa, Oscar Kalowa alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa chanzo ni wamiliki wa mashamba kukataa kikundi kilichopewa leseni kweye mgodi huo kwa madai kuwa kiliaribu mgodi namba moja.

Kalowa aliongeza kuwa wamiliki hao wa mashamba wamegoma kuwaruhusu watu wengine waliopewa leseni kuchimba nje ya mgodi wao, huku wakitaka leseni kwenye mgodi wao wapewe wenyewe.

Aidha, Afisa madini huyo alisema kuwa ofisi yake imeshauri ili kumaliza mgogoro huo, wamiliki hao wa mashamba wapewe leseni kama ambavyo walitaka ili shughuli za uchimbaji ziweze kuendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles