23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Azam imeshusha kipa Mganda

Na Winfrida Mtoi, Dar es Salaam

Klabu ya Azam FC imesajili kipa mpya, Mathias Kigonya, raia wa Uganda kutoka timu ya Forest Rangers ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili.

Ujio wa kipa huyo unaifanya Azam kuwa na makipa wanne ambao ni David Kisu, Benetict Haule na Wilbol Maseke.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema kipa huyo mpya tayari amejiunga na kikosi kilichoweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania baada ya kuondolewa katika michuano ya Mapinduzi.

“Klabu ya Azam imemsajili kipa Mathias Kigonya raia wa Uganda kwa mkataba wa miaka miwili, kuongeza nguvu, ni kipa ambaye amefanya vizuri Zambia kwa misimu miwili yote amekuwa kipa bora wa msimu,” amesema Zaka.

Zaka amesema timu inaendelea kusalia Zanzibar hadi Januari 22, mwaka huu na kucheza mechi tatu za kirafiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles