23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZEE KIGOMA WAMWACHIA MUNGU SPIKA KUMZIBA MDOMO ZITTO

Wazee wa Chama cha ACT Wazalendo, Mkoa wa Kigoma, endapo Spika wa Bunge, Job Ndugai atatekeleza azma ya  kumkataza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuzungumza bungeni watamshtakia Mungu.

Pamoja na mambo mengine, wazee hao wamesema wamesikitishwa na kauli hiyo ya Spika na wamemruhusu Zitto kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya kumsikiliza kwa kina na kujiridhisha.

“Baada ya kusikia kauli za Spika dhidi ya Zitto, tulihitaji kufahamu sababu na kiini cha tatizo lililotokea, hivyo tulimuomba kijana wetu kurejea nyumbani Kigoma kuja kutueleza kabla ya kwenda kwenye kamati ili tupate fursa ya kufahamu kilichotokea,” imesema sehemu ya taarifa ya wazee hao.

Kwa mujibu wa taarifa yao waliyoitoa leo Septemba 15, wazee hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusema kitendo cha Spika kutoa kauli ya kumzuia Zitto kuzungumza katika kipindi chote cha ubunge wake ni kuwazuia wao na wananchi wa Kigoma kusemewa ndani ya bunge.

“Kitendo cha Spika kutoa kauli hiyo kinaashiria kwamba ameshamhukumu mbunge na kiongozi wetu, kwa hivyo kuitwa kwake kwenye kamati ni kupoteza wakati tu, jambo hili halimtendei haki kijana wetu na halitutendei haki sisi wazee tunaomtegemea atusemee.

“Tumesikitishwa na kauli za Spika Ndugai kwani siku zote sisi wazee wa Kigoma tumekuwa tukimuona na kumchukulia Job kama alivyo mtoto wetu Zitto, wawili hawa wamekuwa na mahusiano mema hata kufikia hatua ya kushiorikiana kwa karibu kwenye mazishi ya mama zao,” wamesema wazee hao.

Spika Ndugai alitoa kauli ya kutishia kumzuia Zitto bungeni kwa kipindi chote cha ubunge wake na asiende popote wakati akizungumza bungeni wiki hii kwa kile alichodai Zitto amemdhalilisha Spika na Bunge kuhusu ripoti ya Tanzanite na Almasi kuwasilishwa serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles