25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAWEKEZAJI WANYEMELEA ‘MASHAMBA YA JPM’

Na Amina Omari-Muheza

HALMASHAURI ya Wilaya ya Muheza imeanza kupokea maombi kwa ajili ya  shughuli za uwekezaji wa kilimo, mifugo na viwanda katika mashamba saba ya mkonge yaliyofutiwa umiliki na Rais Dk. John Magufuli.

Mashamba hayo ambayo yote yapo katika wilaya hiyo, wamiliki wake walishindwa kuyaendeleza kwa shughuli za kilimo hivyo serikali kuamua kuyachukua ili kuyagawa kwa wananchi kwa ajili ya kuyaendeleza.

Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Luiza Mlelwa alisema wanakaribisha wawekezaji wenye nia ya kufanya shughuli za uwekezaji katika wilaya hiyo.

Alisema  baada ya kukamilika mpango wa matumizi bora ya ardhi na  a kubaini maeneo ya uwekezaji,   ni fursa sasa  kwa wenye nia ya kufanya uwekezaji kuwahi nafasi hiyo.

“Tumeshaweka utaratibu wa namna ya umiliki ambao ardhi itabaki kuwa   mali ya halmashauri na mwekezaji atapewa eneo la ardhi kwa ubia na  halmashauri kwa ajili ya kufanya shughuli za uwekezaji pekee,” alisema Mlelwa.

Mkurungenzi huyo alisema katika mpango huo wa matumizi ya ardhi yameainishwa maeneo kwa ajili ya kilimo kwa wananchi wanaoishi karibu na mashamba hayo, ufugaji   na uwekezaji .

Alisema    wananchi wanaoishi karibu na mashamba wataweza  kugaiwa ekari tatu pekee huku akisisitiza kwa wafugaji kufuga kisasa badala ya holela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles