22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

UVCCM YAITAKA BAVICHA KUACHA UCHOCHEZI

Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

UMOJA wa Vijana wa CCM umelitaka Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) kuacha kiherehere, upotoshaji na  uchochezi wenye  kupalilia chuki, uhasama na kuingilia masuala ya intelijensia na upelekezi kuhusu tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na watu wasiojulikana

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema kauli za Bavicha zinatakiwa kulaaniwa kwa vile  zina nia potofu ya kuiyumbisha  jamii  jambo ambalo linapaswa kupuuzwa na Watanzania wapenda amani.

Alidai  kitendo cha Mweyekiti na Katibu Mkuu wake kuvinanga vyombo vya usalama na Serikali huku wakidai kuna mfumo kandamizi, si tu   ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu  bali pia ni matamshi yasiyo na staha.

“Tukio la kushambuliwa Lissu  si jambo dogo na jepesi kama  linavyochukuliwa na Bavicha, viongozi wake walipaswa kupima uzito wa maneno yao kabla kutamka  kwa kulinganisha na thamani ya amani, heshima na utulivu uliopo,” alisema Shaka.

Alisema yapo matukio mengi ya ujambazi   yaliyotokea na mengine yamekatisha maisha ya viongozi wa Serikali na kukatisha uhai wao kabla ya hili.

“Amepigwa risasi Rais wa Kwanza wa Zanzibar,  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume akapoteza maisha, ameuawa aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Muungano, marehemu Nickas Mahinda, yote ni matukio ya kupigwa risasi,” alisema.

Matukio ya ujambazi yanayofanywa na watu wasiojulikana  ni mambo yanayotokea hata katika mataifa makubwa na baadhi ya matukio upelelezi wake huchukua miaka na muda mrefu hadi wahusika kutambuliwa au kukamatwa.

Shaka alitoa mfano wa Marekani ambako marais wawili kutoka familia moja  ya kina F.Kennedy  ambaye aliuawa katika mazingira ya  uhalifu lakini pia Rais Anwar Sadat wa Misri alipigwa risasi akiwa anakagua gwaride

“UVCCM tunawaonya Bavicha  waache kiherehere na uchochezi unaoingilia taratibu za upelekezi hasa kwa masuala mazito yakihusisha maisha ya watu, kushambuliwa au kutekwa na kuyageuza yaonekane ni ya siasa,” alisema Shaka.

Katika kile alichodai ni mshangao  viongozi hao wa Chadema kushindwa kutaja  matukio mfululizo wa mauaji ya viongozi wa CCM na serikali za vijiji huko Kibiti na   kifo cha aliyekuwa mwanachama Chadema, mareemu Chacha  Wangwe.

“Mbowe ametamka matamshi yaliyopevuka katika fikra,  upeo na    siasa tofauti na povu la vijana wake walioonyesha uchanga katika siasa huku wakilitumia tukio hili la huzuni la  kushambuliwa Lissu kuwa ni jukwaa lao la siasa,” alisema.

UVCCM vilevile, imewataka Bavicha kutambua kama wana ujasiri  iwaeleze  Watanzania  ni kina nani waliomuwekea sumu, Dk. Harrison Mwakyembe, ni nani aliyempa sumu Zitto Kabwe na kwa nini washindwe kuhoji vifo vyeye utata vya kina  Profesa Kighoma   Malima au  cha marehemu  Ditopile Mzuzuri.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Itafikia sehemu Watanzania wote tujiulize. Shida ya Wanasiasa na viongozi wa CCM ni ipi. Kushika dola, kukumbatiwa na raisi, kutokujua walifanyalo au? Inatisha, tumechoswa na mawazo na kauli zao hata ubinadamu hamna.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles