25.1 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wavuvi Goziba wamuomba DC Muleba kusimamia usalama wao

Renatha Kipaka, Muleba

Wadau wa Uvuvi katika kata ya Goziba, wilayani Muleba, mkoani Kagera wamemuomba Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Toba Nguvila, kusimamia usalama wao ili waweze kuendesha shughuli zao kwa amani.

Mmoja wa wavuvi hao, Joackim Sayuni, amesema kutokana na migogoro inayoendelea kisiwa cha Goziba imepelekea kuondoa ujirani mwema baina na visiwa jirani vya Ukerewe, hivyo wanapokuwa katika shughuli zao ndani ya Ziwa Viktoria wanapopatwa na tatizo inakuwa vigumu sana kusaidiwa.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila amewahakikishia wadau wa uvuvi kuwa yeye pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo watasimamia hali ya usalama kwani ndio jukumu lao ili kuhakikisha wavuvi wanafanya shunghuli zao kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

“Nawakikishia kuwa mpo salama, pamoja na changamoto ndogondogo mnazokutana nazo, Wilaya inazifahamu na inaendelea kuzitatua ili mfanye shughuli zenu mkiwa na amani. Sekta ya uvuvi ni inachangia mapato ya Serikali kwa asilimia kubwa sana wilaya ya Muleba hivyo sisi kama viongozi wa Wilaya tunaiangalia kwa jicho la karibu,” amesema Nguvila.

Awali, wavuvi hao walilalamikia juu ya kutofahamu mapato na matumizi ya ujenzi wa daraja na kumuomba Mkuu wa Wilaya kuwataka viongozi wasome mapato na matumizi ya fedha za ujenzi wa daraja zilizokusanywa.

Akijibu kero hizo Nguvila ameelekeza mara baada ya uongozi mpya wa Mtandao wa Wavuvi kuchaguliwa, uongozi uliovunjwa wakati wa kukabidhi wasome mapato na matumizi kwa uongozi mpya ili wafahamu yaliyofanyika katika uongozi uliopita.

Amewaasa viongozi watakaochaguliwa waingie kwa lengo la kusaidia wadau wa uvuvi kwa kutatua changamoto zao na sio kusumbua wadau wa uvuvi kwa kuwatoza fedha, kuwapiga na kuwanyanganya bidhaa zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Elias Kayandabila amewasihi sana wadau wa uvuvi kuwa wanapochagua viongozi wa kuwaongoza wahakikishe wanachagua viongozi wanaojishughulisha na masuala ya uvuvi kwani wao ndio wanajua uchungu wa mali zao walizowekeza kwenye uvuvi.

Mkutano huo umefanyika katika kisiwa cha Goziba, ambapo Mkuu wa Wilaya, Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mwakilishi wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Mkurugenzi Mtendaji na wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji walikuwa na ziara ya siku tatu kwa ajili ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo kisiwani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles