28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wasimamishwa kwa ubadhirifu wa mamilioni

Antony-MtakaNa Upendo Mosha, Hai

SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai  kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 70.

Vilevile imemfukuza kazi mhasibu mmoja wa Hospitali Teule ya Machame kwa tuhuma hizo hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Antony Mtaka, alisema jana kuwa watumishi hao wamesimamishwa kazi   baada ya kuthibitika kufanya ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.

Alisema   wawili kati yao ni maofisa wa halmashauri hiyo ambao  wanadaiwa kuhusika na upotevu wa zaidi ya Sh milioni 38.

“Fedha hizo zilikuwa za malipo ya muda wa ziada wa  saa za kazi za watumishi wa Hospitali Teule ya Machame,” alisema.

Mtaka aliwataja watumishi hao   kuwa ni  Valentine Gisha na Edewin Kalokola, ambao wanadaiwa  kushirikiana  na Mhasibu wa Hosptali hiyo, Philipo Massasi.

Alisema Serikali pia imewasimamisha maofisa wawili wa idara ya utumishi wa Halmashauri ya Hai wanadaiwa  kughushi nyaraka za madaktari  waliokwisha kuacha kazi.

Mtaka alidai watumishi hao walitumia nyaraka na majina ya watumishi hao kuchukua mikopo wa zaidi ya Sh milioni 36 kutoka benki  ya CRDB.

Aliwataja watumishi waliohusika na kughushi huko kuwa  ni  Faraja Nandatu na Isaya Buhege.

Alisema   watumishi hao wamekwisha kupewa barua za kusimamishwa kazi na   vyombo  vinavyohusika ikiwamo   TAKUKURU vinaendelea na uchunguzi.

Mtaka alizitaka taasisi za fedha   kujitathimi kuhusiana na watumishi wake ambao baadhi  hushirikiana na watumishi wa serikali   kufanya utapeli.

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Fredy Kweka, alisema watumishi hao wane walisimamishwa kazi   tangu Novemba 11.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles