24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kijo Bisimba afanyiwa upasuaji

Dr-Helen-Kijo-BisimbaVeronica Romwald na Nicodemas Kikwati (GHITBS), Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba, amefanyiwa upasuaji wa mguu  wa kushoto.

Upasuaji huo umefanyika  katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Akizungumza na MTANZANIA jana hospitalini hapo, Dk. Bisimba alisema alifanyiwa upasuaji huo  juzi jioni na   anaendelea vizuri na matibabu.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri, nimefanyiwa upasuaji na madaktari wameniwekea vyuma  kuisaidia mifupa yangu iweze kujishika, naamini nitapona,” alisema.

Alisema ipo haja kwa jamii hususan madereva kuwa makini na kufuata sheria za usalama barabarani kwa sababu  ajali nyingi zinaweza kuepukika.

“Kwa kweli nilishangaa kupata ajali Dar es Salaam tena Jumapili siku ambayo magari huwa si mengi mjini wakati nilitoka na gari lile Mlimba (Morogoro).

“Ajali ile ilitokea kwa sababu dereva aliyetugonga hakuwa makini, alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi.

“Pale  tulikuwa kwenye makutano ya barabara   na taa zilituruhusu, gari ya mbele yetu ilipita na sisi tulipotaka kupita ndipo alipotugonga,” alisema.

Dk. Bisimba alisema alifarijika   alipotembelewa na Rais Dk. John Magufuli katika Hospitali ya Agha Khan  ambako alikuwa amelazwa awali.

Dk. Bisimba alipata ajali Novemba 8  mwaka huu kwenye  taa za Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles